WAZIRI MKUU: TIMU YA MAWAZIRI WANANE INAHUSIKA NA MIGOGORO MIKUBWA TU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema timu ya mawaziri wanane kutoka wizara shiriki inashughulikia migogoro mikubwa tu ya ardhi ambayo hulazimu kukutanisha wataalamu kutoka wizara husika. Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 19, 2022) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mbarali, Bw. Francis Mtega kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu